Katika kikao cha 22 cha Umoja wa Mataifa cha Watu wa Asili kinachofanyika Jijini New York Marekeni Tanzania imepata fursa ya kutoa ufafanuzi juu ya mgogoro wa Ngorongoro wa Wamasai Mkoani Manyara.
Ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Prof. Hamisi Malebo ambaye ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO umeileza Dunia kwamba Tanzania inaheshimu na kuthamini maisha na haki ya kila mtanzania ikiwa ni pamaoja na wajibu wa kuhakikisha kila mtanzania ananufaika na rasilimali za nchi katika jitahada za kujiletea maendeleo.
Aidha, ujumbe huo ulisema kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina makabila yapatayo 120 na kwamba makabila yote yana haki sawa ya kufaidika na kila aina ya rasilimali iliyopo kwa vizazi vilivyopo na vijavyo. Prof. Hamis Malebo akitoa ufafanuzi juu ya kile kinachoitwa watu wa asili nchini Tanzania, ameeleza kuwa Tanzania haijawahi kuwa na watu wa asili kwa kuwa ilianza kukaliwa takribani miaka 5000 iliyopita na watu kutoka makundi ya Kushi na Khosai wajulikana leo kama Wabantu na baadae watu wenye asili ya Nilotic walianza kuingia katika eneo hili linalojulikana leo kama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia karne ya 18 ikiwa ni pamoja na Wamasai. Taarifa ya Tanzania iliwasilishwa na Afisa Mwandamizi wa uwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Bi. Zulaikha Tambwean
Kadhalika, Prof. Malebo akiongea na Mwandishi Maalum wa Jukwaa la Watu wa Asili Bw. Cali T zay kutoka Guatemala alimwarifu kuwa Tanzania imekuwa na inaendelea kushughulikia kero mbalimbali za jamii ya Wamasi ikiwa ni pamoja na kuandaa mazingira mazuri ya kuishi na kupata huduma sitahiki kama jamii zingine za kitanzania. Pia Prof. Malebo alimuomba mwandishi huyo apatapo nafasi atembelee Tanzania hususani jamii ya kimasai ili kujionea jitihada zinazofanywa na serikali katika kuimarisha ustawi wa Wamasai