Tume ya Taifa ya UNESCO kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imetekeleza mradi wa maji wa kidigital unaotumia mionzi ya Jua kuyatibu maji . na kuyafanya maji hayo kuwa salama kwa matumizi ya Binadamu katika kata ya Katoma, wilaya ya Geita Mkoani Geita. Mradi huu wenye jina la .“Universal Access to Safe Drinking Water, Hygiene and Sustainable Sanitatation(WASH) in Rural Community”. unaotumia tekinolojia, ubunifu yenye lengo la kumtua Mama ndoo kishwani kwa Hisani ya Raisi Samia Suluhu Hassan ya maji salama kuwafikia watanzania wa vijijini ambao hawajafikiwa na Maji ya bomba.
Mbali na kujenga miundombinu ya mabomba, ujenzi wa vichoteo vya maji (Distributing Points) kwa kuweka hifadhi ya matenki manne (4),Tume ya taifa ya UNESCO imeweza kubuni mfumo wa MajiPesa control box unaofungwa kwenye kila kichoteo ambapo mwananchi huweza kuchangia pesa kidogo ili kupata huduma ya maji na kuufanya mradi uwe endelevu.
Aidha Mfumo huu unauwezo wa kutuma ujumbe kwa wajumbe wote wa kamati ya maji ngazi ya jamii ( community-based water suppy organization-CBWSO) na mamlaka za maji RUWASA-Geita.